27 Julai 2026 - 21:26
Ayatollah Asad Qasir Al-‘Amili: Mazungumzo ya Amani na Marekani Yanapingana na Kanuni za Qur’an na Sharia ya Kiislamu

Ayatollah Asad Qasir Al-‘Amili amesema kuwa, ingawa msingi wa mahusiano na wasiokuwa Waislamu ni amani, wema na uadilifu, amani haiwezi kukubaliwa ikiwa imejengwa juu ya dhulma au udhalilishaji. Amesema pia kuwa adui ambaye amevunja mikataba mara kadhaa hawezi kuaminika katika makubaliano ya amani, na kwamba hali ya Marekani inaangukia katika misingi hiyo.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - AyatoMujallah Asad Muhammad Qasir Al-‘Amili ameeleza msimamo wa kisheria wa Qur’ani kuhusu suala la amani na maridhiano na Marekani, akisisitiza kuwa mazungumzo ya amani yanapaswa kuzingatia misingi ya uadilifu, heshima na kutokuwepo kwa dhulma au udhalilishaji.

Katika kueleza msimamo huo, Ayatullah Qasir Al-‘Amili amesema kuwa msingi wa mahusiano ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu ni amani na kuwatendea kwa wema. Ikiwa hilo haliwezekani, basi ni lazima angalau kuwatendea kwa uadilifu.

Amebainisha kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:


﴿لَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴾[سورة ممتحنة، آیة ۸]

Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na kuwaadilifu wale ambao hawakupigana nanyi kwa sababu ya Dini, wala hawakukutoeni katika makazi yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kufanya uadilifu.” (Surat Al-Mumtahanah, 8)
 

Aidha, amesema kuwa ikiwa kundi la wasiokuwa Waislamu litapigana na Waislamu, ni wajibu kujilinda. Hata hivyo, ikiwa upande huo utaelekea kwenye amani na ukweli wa nia yake ukathibitika, basi amani inaweza kukubaliwa.

Kwa mujibu wa Ayatullah Qasir Al-‘Amili, amani hiyo lazima ijengwe juu ya msingi wa uadilifu. Amesisitiza kuwa amani inayojengwa juu ya dhulma yenyewe inakuwa aina ya dhulma, hivyo si halali kufanya amani na mtu yeyote ikiwa makubaliano hayo yamejengwa juu ya udhalilishaji au dhulma.

Katika nukta nyingine, amesema kuwa ikiwa adui ambaye amewahi kupigana na Waislamu ataelekea kwenye amani, lakini hapo awali amefanya mikataba mara kadhaa ya kutovamia na kisha akawa anavunja mikataba hiyo mara kwa mara, basi suala hilo linahitaji kuchukuliwa kwa mtazamo tofauti.

Amesema kuwa kwa mujibu wa Aya za Qur’ani zinazohusiana na Jihadi na mapambano, adui mpiganaji ambaye amevunja mikataba zaidi ya mara moja hawezi kuaminika katika makubaliano ya amani, na kwamba mapambano dhidi yake yanaweza kuendelea mpaka ajisalimishe.

Miongoni mwa Aya alizozitaja ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:


﴿وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ﴾

Na waueni popote mtakapowakuta.” (Al-Baqarah: 191)


Pamoja na kauli nyingine:


﴿وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ﴾

Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina.” (Al-Baqarah: 193)


Katika hitimisho la msimamo huu wa Kiislamu, Ayatollah Asad Muhammad Qasir Al-‘Amili amesema kuwa Marekani inaangukia katika kanuni ya pili na ya tatu alizozieleza. Kwa hiyo, kwa mtazamo huo wa Kiislamu, kufanya mazungumzo na Marekani kwa lengo la amani na maridhiano kunapingana na kanuni za Qur’an na hukumu za Sharia ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha